array(0) { } Radio Maisha | Zaidi ya asilimia 68 ya wakazi wa jiji la Lombardy, Italia waripotiwa kufariki kutokana na korona

Zaidi ya asilimia 68 ya wakazi wa jiji la Lombardy, Italia waripotiwa kufariki kutokana na korona

Zaidi ya asilimia 68 ya wakazi wa jiji la Lombardy, Italia waripotiwa kufariki kutokana na korona

Tangu kuzuka kwa virusi vya korona jijini Wuhan, Uchina, taifa la Italy limesalia katika vichwa vya habari kwa kuongoza kwa idadi ya vifo na maambukizi ya virusi hivyo.

Utafiti kwenye mitandao na majarida ya Italy umebainisha kwamba mji wa Lombardy ndio ulioathirika zaidi na vifo vilivyotokana na virusi vya korona. Zaidi ya asilimia 68 ya wakazi wa mji huo wameripotiwa kufariki dunia.

Kwa sasa serikali ya Italy inalaumiwa kwa kuzingatia pakubwa kuwapima wanaoshukiwa kuugua badala ya kuwatibu waliokuwa wakiugua.

Hata hivyo, utafiti umebainisha kuwa mataifa ya Italy na Uchina yana uhusiano wa karibu wa miaka mingi katika sekta ya viwanda vya nguo hususan Mkoa wa Wuhan ambako wafanyakazi zaidi ya laki moja raia wa Uchina wameajiriwa Kaskazini mwa Italy katika viwanda hivyo.

Inaarifiwa kwamba wafanyakazi hao wa Uchina walisafiri kutoka Italy kuelekea nyumbani mapema mwaka huu kati ya tarehe 25 na Februari 8 kusherehekea mwaka mpya na familia zao na huenda waliporejea walichangia kusambaza virusi hivyo ikizingatiwa kwamba hawakupimwa walipotua nchini Italy.