array(0) { } Radio Maisha | Watu watatu kutoka Kenya wathibitishwa kuwa na korona nchini Rwanda

Watu watatu kutoka Kenya wathibitishwa kuwa na korona nchini Rwanda

Watu watatu kutoka Kenya wathibitishwa kuwa na korona nchini Rwanda

Watu watatu waliosafiri kutoka humu nchini hadi Rwanda ni miongoni mwa waliotangazwa kuambukizwa virusi vya korona na serikali ya taifa hilo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini Rwanda, kuna maambukizi mapya 17 hivyo kufikisha 36 idadi ya walioathiriwa. Miongoni mwa kumi na saba hao wapya, watatu walitoka Kenya, 9 kutoka Dubai, wawili kutola Marekani, mmoja Qatar na mwingine India. Aidha, mwingine aliyeambukizwa ni mtu aliyetangamana na mmoja wa waathiriwa.

Kufikia sasa watu 16,558 wamefariki kote duniani huku wengine 381,761 wakiambukizwa. Ilivyo sasa, watu 12,062 miongoni mwa walioambukizwa wako katika hali mahututi.