array(0) { } Radio Maisha | Wafanyakazi wote wa Idara ya Mahakama kufanyia kazi nyumbani ili kuzuia Korona

Wafanyakazi wote wa Idara ya Mahakama kufanyia kazi nyumbani ili kuzuia Korona

Wafanyakazi wote wa Idara ya Mahakama kufanyia kazi nyumbani ili kuzuia Korona

Maafisa wote wa Idara ya Mahakama wameagizwa kufanyia kazi nyumbani huku kesi za dharura zikishughulikiwa kupitia baruapepe ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona. Agizo hilo limetolewa na Msajili wa Idara ya Mahakama, Anne Amadi.

Kupitia notisi, Amadi amesema kuwa wafanyakazi wa idara hiyo wamekuwa wakilalamikia namna wanavyotangamana na wananchi licha ya kupunguzwa kwa shughuli za mahakama. Idara ya Mahakama imesema baada ya kutathmi masuala yaliyoibuliwa, imefanya kipaumbele usalama wa wafanyakazi wake.

Kutokana na hali hiyo, wakuu wote wa mahakama wameagizwa kuweka notisi katika mahakama wanazohudumu ili kuufahamisha umma kuhusu suala hilo.

Awali, Jaji Mkuu alitoa agizo kuhusu namna shughuli zingeendeshwa katika Idara ya Mahakama. Miongoni mwa maagizo hayo yalikuwa, kila kituo cha mahakama kusalia na wafanyakazi watatu pelee na jaji au hakimu mmoja tu.

Wakenya kutoruhusiwa kuingia katika majengo ya mahakama badala yake kuwasilisha kesi za dharura, wafungwa kutowasilishwa gerezani na wahalifu wapya kushughulikiwa katika vituo vya polisi.