array(0) { } Radio Maisha | Raila amekana madai kwamba alitangamana na Naibu Gavana wa Kilifi, Gideon Saburi ambaye ameambukizwa korona

Raila amekana madai kwamba alitangamana na Naibu Gavana wa Kilifi, Gideon Saburi ambaye ameambukizwa korona

Raila amekana madai kwamba alitangamana na Naibu Gavana wa Kilifi, Gideon Saburi ambaye ameambukizwa korona

Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga, amekana madai kwamba alitangamana na Naibu Gavana wa Kilifi, Gideon Saburi ambaye ameambukizwa korona, huku akiitaka serikali kuwanaswa na kuwashtaki wanaoeneza propaganda kuhusu virusi hivyo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Dennis Onyango, Odinga amekiri kwamba alizuru eneo la Pwani juma lililopita lakini amepuuza tetesi za kukutana na Saburi akitaja madai hayo kuwa uongo.

Odinga amesema kuwa alikutana na Naibu Gavana wa Mombasa Dakta William Kingi pekee na kutumia muda wote kupumzika huku akiwataka Wakenya kupuuza uvumi huo akitaka wanaotumia mitandao ya kijamii kueneza uvumi kuhusu korona kunaswa na kushtakiwa.

Odinga aidha amesema amekuwa akizingatia maagizo ya Serikali Kuu kuhusu korona tangu kisa cha kwanza kiliporitiwa humu nchini Machi 13 hasa kupiga marufuku mikutano ya umma.

Wakati uo huo, amewahimiza Wakenya kuendelea kutilia maanani mwongozo wa serikali ili kupunguza maambukizi ya korona nchini.

Saburi ameendelea kukashifiwa na Wakenya baada ya kupuuza sharti la kujitenga kwa yeyote anayeingia nchini kutoka mataifa ya kigeni yaliyoathirika huku serikali ikisema atashtakiwa atakapomaliza kipindi cha karantini.

Saburi anasemakana kutangama na wafanyakazi wa kaunti na hata kufanya mikutano kinyume na sheria alipotoka Ujerumani hivyo kuhatarisha maisha ya Wakenya. Aidha safari za ngeze la kimataifa zitapigwa marufuku kuanzia Jumatano wiki hii.