array(0) { } Radio Maisha | Serikali kuboresha huduma za mitandao ili kurahisisha shughuli za Wakenya wakiwa nyumbani

Serikali kuboresha huduma za mitandao ili kurahisisha shughuli za Wakenya wakiwa nyumbani

Serikali kuboresha huduma za mitandao ili kurahisisha shughuli za Wakenya wakiwa nyumbani

Serikali imetangaza mikakati ya ziada ya kuhakikisha wanafunzi walio nyumbani kufuatia janga la korona wanaendelea na masomo yao kupitia njia ya mtandao vilevile Wakenya kuendelea kufanya kazi wakiwa nyumbani.

Akilihutubia taifa muda mfupi uliopita, Rais Uhuru Kenyatta amesema Mamlaka ya Safari za Angani imeafikiana na Kampuni ya Google Loon kwa ushirikiano na ile ya Telkom Kenya kuboresha huduma za mitandao ili kuwarahisishia Wakenya shughuli zao, kufuatia agizo la serikali la kuwataka Wakenya kufanya kazi wakiwa nyumbani, inapokabili Korona.

Kenyatta amesema mpango huo utalisaidia taifa katika kukabili maambukizi zaidi ya Korona kwa kuwa itasaidia idadi ya watu katika maeneo mbalimbali hivyo basi kudhibiti kusambaa kwa virusi vya korona.

Kuhusu wanafunzi ambao wako nyumbani kufuatia agizo la kufungwa kwa taasisi zote za elimu nchini katika juhudi za kukabili korona, Kenyatta amesema mpango huo wa huduma za mtandao utawasaidia walimu kuwasiliana nao na hata kuendeleza masomo.

Amesema mpango wa masomo kupitia vipindi vya redio vilevile kupitia mitandao ya Taasisi ya Ukuzaji MtalaaKICD, utafanikishwa na huduma hizi.

Kenyatta amesema uamuzi huu umeafikiwa ili kulinda haki za wafanyakazi ambao kufikia sasa wengi wao wanaendelea kutekeleza majukumu yao wakiwa nyumbani.

Ikumbukwe serikali iliyazishauri kampuni nchini kupunguza idadi ya wafanyakazi ili kukabili kusambaa kwa korona. Awali ilitangaza kufungwa kwa taasisi zote za elimu na kuwataka wanafunzi kurejea nyumbani.