array(0) { } Radio Maisha | Robert Alai aachiliwa kwa dhamaana
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Robert Alai aachiliwa kwa dhamaana

Robert Alai aachiliwa kwa dhamaana

Mwanablogu mwenye utata Robert Alai amefikishwa katika Mahakama ya Milimani ambapo amefunguliwa mashtaka ya kuchapisha taarifa za uongo kuhusu Virusi vya Korona.

Aidha, Alai amefunguliwa shtaka jingine kwa kuchapisha katika mtandao wake wa Twitter kwamba serikali inaficha ukweli kuhusu virusi hivyo hatari duniani.

Mbele ya Hakimu Muema Ndungi, Alai ametuhumiwa kwa kuchapisha taarifa hizo kinyume na kipengee cha ishirini na tatu ya ukiukaji wa utumizi wa mitandao.

Alai alikamatwa Ijumaa wiki iliyopita baada ya kuhojiwa kwa muda wa saa tano katika Idara ya Upelelezi, DCI.

Kukamatwa kwake kunajiri baada ya Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe kuonya kwamba yeyote atakayetoa taarifa zisizothibitishwa kwa umma kuhusu virusi hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha, Kagwe alionya kwamba wote wanaohusishwa na taarifa hizo watakamatwa kisha kupelekwa katika Hospitali ya Mbagathi walikolazwa wagonjwa wote wa Covid-19 kisha kushinikizwa kuripoti wanachoona wakati huo.

Wakati uo huo, wanahabari na Wakenya wanaoeneza uvumi kuhusu virusi hivyo walionywa dhidi ya kufanya hivyo kwani wanazua hofu nchini.

Alai amekana madai hayo huku akiachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu hamsini pesa taslimu au bondi ya shilingi laki moja unusu.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 23 mwezi Aprili mwaka huu.