array(0) { } Radio Maisha | Kenny Rogers ameaga dunia
Kenny Rogers ameaga dunia

Mwanamziki maarufu Kenny Rogers amefariki dunia. Kulingana na familia yake Rogers anayetamba kwa nyimbo za mtindo wa Country amefariki dunia akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda mrefu hali yake ikadorora kufuatia umri wake .

Rogers ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka themanini na mmoja alistaafu mwaka 2017.  Kando na Mtindo wa Country marehemu pia aliimba nyimbo za mitindo ya Jazz, Folk, na Pop.

Anakumbukwa kwa vibao vyake maarufu kama vile Gambler, Coward of the Country na Lady vilivyotamba sana miaka ya 70 na 80 na vinaendelea kutamba hadi sasa.  Hiki hapa ni kionjo cha baadhi ya nyimbo zake.

Marehemu Rogers aliendeleza umaarufu wake kwa kuwashirikisha wanamziki wengine kama vile Dolly Patron na aliwahi kushida tuzo za Grammy mara tatu. Kando na Mziki anakumbukwa katika fami ya uiigizaji.

Marehemu amemwacha mjane Wanda Miller mwenye umri wa miaka hamsini na minne na wanao pacha Jordan na Justin wenye umri wa miaka kumi na minne.

Aidha Kenny ni baba wa watoto wengine watatu ambao ni   Carole, mwenye umri wa miaka sitini , Kenny Jr, mwenye umri wa miaka hamsini na mitano 55 na Christopher Cody, mwenye umri wa miaka  37 kutoka kwa ndoa zake za awali kwani alioa na kufanya harusi mara tano kabla ya kumwoa mewe Miller mwaka 1997.

Kufuatia janga la Virusi vya Korona familia hiyo imesema hafla ya mazishi haitausisha umma japo imeahidi ibada ya maombi itafanyika baadaye.

Mungu ailaze roho yake mahali pema palipo wema.