array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya Wakenya wanaougua Korona ingali 7
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idadi ya Wakenya wanaougua Korona ingali 7

Idadi ya Wakenya wanaougua Korona ingali 7

Na Esther Kirong'

NAIROBI, KENYA, Watu wengine wanne wamelazwa katika Hospitali ya Mbaghathi kwa kushukiwa kuwa na Virusi vya Korona japo mmoja miongoni mwao amebainika kutougua huku wengine watatu wakisubiri matokeo.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kufikia sasa bado ni watu 7 ambao wameambukizwa huku waliotangamana nao wakiendelea kufuatiliwa.

Waziri Kagwe aidha amesema matokeo ya mtu mwingine aliyetegwa katika Kaunti ya Kilifi yatatolewa kesho asubuhi.

Aidha, ikizingatiwa kwamba virusi hivyo huchukua siku 14 hivi kuonekana mwilini na hata kusababisha dadili, Kagwe amebashiri kuwa huenda hali ikawa mbaya hata zaidi kuanzia wiki ijayo kwa kuzingatia mkondo wa mambo katika mataifa yaliyoathirika.

Kagwe ametangaza mikakati zaidi ya kuzuia hali hiyo kushuhudiwa nchini. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kufungwa kwa baa zote na maeneo ya burudani kufikia saa moja unusu usiku.

Waziri Kagwe hata hivyo ametangaza kwamba masoko hayatafungwa sasa ili kuwaruhusu watu kuendelea kupata bidhaa muhimu japo ni lazima yasafishwe mara kwa mara huku soko la Gikombaa likitarajiwa kusafishwa kesho.

Magari ya kuwabeba abiria 14 aidha yameagizwa kuwabeba abiria wanane pekee ili kuhakikisha watu hawakaribiani wanaposafiri. Vile vile magarimoshi na mabasi yameagizwa kupunguza idadi ya abiria ili kuzuia maambukizi.