array(0) { } Radio Maisha | Wakenya mbalimbali kupimwa virusi vya korona
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakenya mbalimbali kupimwa virusi vya korona

Wakenya mbalimbali kupimwa virusi vya korona

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Miongoni mwa mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani WHO ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Korona, ni kwa mataifa hasa Barani Afrika kuwafanyia ukaguzi wananchi. Ni kufuatia wito huu ambapo serikali imetangaza kwamba kuanzia Jumamosi maafisa wa afya watakuwa wakiwapima watu katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema maafisa hao watashirikiana na wale wa Shirika la Msalaba Mwekundu katika shughuli hiyo, hatua ambayo inalenga kuwatambua watu waioambukizwa ili hatua madhubuti zichukuliwe.

Aidha, amesema viongozi wa nyumba kumi watahusishwa katika kuifuatilia mienendo ya wananchi kubaini iwapo wanazingatia masharti ya kujikinga yaliyotolewa na serikali.

Humu nchini, kufikia sasa visa vya walioambukizwa vimesalia saba huku watu mia moja arubaini na watano waliotangamana na walioambukizwa wakitambuliwa.

Kwa mujibu wa Waziri Kagwe ni kwamba uchunguzi zaidi unaendelea kwa watu saba walioambukizwa kubaini iwapo kuna yule ambaye amepona kufikia sasa. Miongoni mwa saba hao, sita ni raia wa Kenya na mmoja Mburundi.

Aidha, watu takriban laki sita wamekaguliwa kufikia sasa,  baada ya kuingia nchini ili kuhakikisha walioathiriwa wanatambuliwa kwa wakati.

Tayari serikali imeanza kuwapa watu wanaoingia humi nchini kutoka mataifa ya kigeni fomu maalum ambayo watatia saini kuahidi kwamba watajitenga kwa siku kumi na nne na watakapopatikana wakikiuka agizo hilo la serikali watakamatwa na kushtakiwa.