array(0) { } Radio Maisha | Mafunzo ya kuigwa kuhusu kukabili virusi vya korona

Mafunzo ya kuigwa kuhusu kukabili virusi vya korona

Mafunzo ya kuigwa kuhusu kukabili virusi vya korona

Na Mate Tongola,

NAIROBi, KENYA, Taifa la Italia limeendelea kuathirika zaidi kufuatia idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na maambukizi ya Virusi vya Korona. Katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita,  jumla ya watu mia nne ishirini na saba wamefariki dunia hivyo basi kufikisha elfu tatu mia nne na tano jumla ya watu waliofariki dunia Italia kufuatia Korona.

Idadi hii ni ziadi ya waliofariki Uchina taifa lililoathirika zaidi na janga hilo.

Hayo yanajiri, huku kwa siku ya pili leo hii hakuna kisa kipya cha maambukizi ya Korona kilichoripotiwa Uchina, huku madaktari wake wakitumwa katika taifa la Italia kusaidia kudhibiti hali.

Uchina iliweka mikakati kadhaa kuhakikisha kwamba maambukizi zaidi yanazuiwa kukiwamo kudhibiti idadi ya watu wanaoruhusiwa kutoka nje kwa wakati, vile vile kupiga marufuku mikutano ya hadhara, kufungwa kwa maeneo ya burudani na hata yale ya kuabudu.

Loghan Machoka mwanafunzi wa Chuo kimoja Kikuu kilichoko Uchina ameileza Radio Maisha jinsi serikali ya Uchina ilivyoimarisha miakakati yake.

Si hayo tu, Serikali ilihakikisha inawakagua raia wote wanaoishi nchini humo ili kuzuia maambukizi zaidi. Kwa mujibu wa Loghan,  shughuli za kawaida zimeanza kurejelewa japo wananchi wanaimizwa kuwa makini.

Kando la Italia na Uchina,  Iran ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika zaidi huku idadi ya waliofariki dunia ikifikia elfu moja mia mbili themanini na nne.

Hayo yanajiri huku Tovuti ya Growth Factor of Novel , ikichapisha kuwa watu elfu 10 na 48 wamefariki dunia kote duniani kufikia leo Machi 20 mwendo wa saa nane usiku. Idadi hii imeongezeka kutoka jana ambapo watu 9,377 walitangazwa kufariki dunia.

Aidha tovuti hiyo imesema kuwa watu elfu 245, 613 wameambukizwa kwenye mataifa 179 kote duniani.