array(0) { } Radio Maisha | Modern Coast yasitisha safari za nje ya nchi

Modern Coast yasitisha safari za nje ya nchi

Modern Coast yasitisha safari za nje ya nchi

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Kuhusu suala lilo hilo la Korona, mashirika mbalimbali yanaendelea kuimarisha mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo hadi humu nchini.

Kampuni ya mabasi ya Modern Coast imesitisha kwa muda safari zake kuelekea mataifa jirani ya Tanzania, Uganda na Rwanda hadi pale janga hilo litakapodhibitiwa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari , usimamizi wa kampuni hiyo umesema shughuli zake kwenye mataifa hayo zitarejelewa pale maambukizi ya Korona yatakapopungua.

Wateja na abiria wote ambao wameathirika wameshauriwa kuzitembelea ofisi za kampuni hiyo kurejeshewa pesa zao au kuahirisha safari.