array(0) { } Radio Maisha | Mudavadi atoa wito wa kupunguzwa kwa bei za bidhaa muhimu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mudavadi atoa wito wa kupunguzwa kwa bei za bidhaa muhimu

Mudavadi atoa wito wa kupunguzwa kwa bei za bidhaa muhimu

Na Caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Kiongozi wa Chama cha ANC, Musalia Mudavadi ameitaka serikali kupunguza bei ya bidhaa muhimu na kuondoa kodi kwa bidhaa hizo ili kuwanufaisha Wakenya wakati huu ambapo taifa linapambana na maambukizi ya Virusi vya Korona.

Mudavadi amesema Kenya inastahili kuiga mifano ya mataifa mengine kama vile Marekani ambayo imeondoa kodi kwenye bidhaa muhimu kuwawezesha wananchi kujimudu.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Mudavadi amesema ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa taasisi za afya nchini hazikumbwi na uhaba wa dawa na vifaa muhimu.

Aidha amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kuwaagiza wamiliki wa nyumba za kupanga kutowafurusha wapanganji kutokana na kodi za nyumba mbali na kulinda biashara za Wakenya.

Wakati uo huo, ametoa wito wa kufadhiliwa kifedha kwa waagizaji wa bidhaa kutoka mataifa ya kigeni huku pia akiipongeza serikali kwa juhudi za kuvikabilivi Virusi vya Korona nchini.

Haya yanajiri huku Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri KUPPET, ukitoa wito kwa serikali kuwalinda walimu dhidi ya Virusi vya Korona kwa kuwalipia bima ya matibabu.

Mwenyekiti wa KUPPET Omboko Milemba ameiomba serikali kutoa malipo ambayo walimu wanadaiwa ili kuwawezesha kupata matibabu endapo wataambukizwa Virusi vya Korona na magonjwa mengine.

Nayo, Mamlaka ya Kutathimini Utendakazi wa polisi, IPOA imemtaka Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai kuagiza kuachiliwa mara moja kwa washukiwa mbalimbili ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Korona.

Mwenyekiti wa IPOA, Anne Makori amesema kuwa Mutyambai ni sharti ahakikishe kuwa wasimamizi wa vituo OCS, wanawaachilia washukiwa kwa bondi ya polisi pasi na masharti.