array(0) { } Radio Maisha | Magaidi 12 wauliwa kwenye Kaunti ya Lamu

Magaidi 12 wauliwa kwenye Kaunti ya Lamu

Magaidi 12 wauliwa kwenye Kaunti ya Lamu

Na Caren Omae,

NAIROBi, KENYA, Jeshi la Ulinzi KDF limefanikiwa kuwauwa washukiwa kumi na wawili wa kundi Gaidi la Al-Shabaab kwenye eneo la Nginda linalopatikana kati ya Korisa na Bargoni. Inaarifiwa kumi na wawili hao wameuliwa baada ya jaribio lao la kivamia  kambi ya Jeshi kwenye eneo hilo kutibuka.

Miongoni  mwa waliouliwa ni mshukiwa ambaye ni kamanda wa kundi hilo kutoka eneo la Pwani ambaye amekuwa akitoa tarifa vilevile uangalizi wa magaidi hao ambao wamekuwa wakijificha katika msitu wa Boni.

Wakati wa oparesheni hiyo, maafisa wa KDF wamefanikiwa kumkamata mshukiwa mmoja akiwa hai, bunduki tatu aina ya AK 47, maganda saba ya risasi, zaidi ya risasi elfu moja na chombo cha kubebea maji.

Mafisa hao wa KDF wamekuwa wakipendekeza msako tangu Machi 13  baada ya Al-Shabaab  kushambulia kambi ya Kitole Special Operations Group.