array(0) { } Radio Maisha | KQ yawahakikishia abiria wake usalama wa kiafya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

KQ yawahakikishia abiria wake usalama wa kiafya

KQ yawahakikishia abiria wake usalama wa kiafya

Na Esther Kirong'

NAIROBI, KENYA, Shirika la Ndege la Kenya Airways, KQ limefafanua kuhusu kisa ambapo abiria wanne raia wa Japan waliokuwa wameabiri ndege jijini Nairobi kuelekea Sierra Leone Jumatano walizuiwa kuingia nchini humo kwa madai ya mmoja wao kuambukizwa Virusi vya Korona.

Kenya Airways imesema kwamba abiria hao ambao walikuwa wametoka Amsterdam kisha kuja Kenya ili kuendelea na safari hadi Sierra Leone, walikuwa wamefanyiwa ukaguzi wa kiafya unaohitajika katika Uwanja wa Ndege wa JKIA.

Hata hivyo maafisa wa uhamiaji nchini Sierraleone waliagiza warejeshwe walikotoka. Kq  imesema abiria hao walifanyiwa ukaguzi kwa mara nyingine baada ya kurejeshwa Kenya na kuidhinishwa kusafiri.

Shirika hilo limesema wataruhusiwa kuabiri ndege nyingine kurejea walikotoka huku likiwahakikishia abiria kwamba linashirikiana kwa karibu na wahudumu wa afya kuhakikisha usalama wa kiafya wa abiria unazingatiwa.