array(0) { } Radio Maisha | Unyunyiziaji dawa katika vituo vya mabasi Jijini Nairobi wang'oa nanga

Unyunyiziaji dawa katika vituo vya mabasi Jijini Nairobi wang'oa nanga

Unyunyiziaji dawa katika vituo vya mabasi Jijini Nairobi wang'oa nanga

Na Beatrice Maganga,

NAIROBI, KENYA, Wizara ya uchukuzi kwa ushirikiano na ile ya Afya inaongoza shughuli ya unyunyiziaji dawa katika vituo vya mabasi jijini Nairobi ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Korona. Shughuli hiyo imeanzia katika kituo cha mabasi ya Kencom ambapo mabasi yote ya abiria yatanyunyiziwa dawa.

Ikumbukwe ni jana pia Kaunti ya Nairobi ilizindua shughuli ya unyunyuziaji wa dawa katikati ya jiji hili na viunga vyake.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya katika Kaunti hii, Wilson Langat alisema mashine maalum za kunyunyiza dawa hiyo zitafungwa kwa magari ambayo yatazunguka jijini kutekeleza shughuli hiyo na kwamba familia za mitaani vilevile zitahusishwa.

Hatua hii inajiri siku kadhaa baada ya Serikali ya Kitaifa kutekeleza shughuli ya unyunyuzaji wa dawa mtaani Rongai baada ya kuripotiwa kwamba mwanamke aliyepatikana na ugonjwa wa Covid-19 alikuwa akiishi eneo hilo.