array(0) { } Radio Maisha | Itumbi miongoni mwa maafisa waliotemwa na PSC

Itumbi miongoni mwa maafisa waliotemwa na PSC

Itumbi miongoni mwa maafisa waliotemwa na PSC

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Mkuu wa Kitengo cha Dijitali katika ofisi ya rais ni miongoni mwa watu watano waliofutwa kazi kufuatia hatua ya Tume ya Huduma za Umma PSC kuziondoa baadhi ya nyadhfa.

Kulingana na PSC kitengo hicho hakihitajiki tena.

Nyadhfa nyingine zilizooondolewa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano ya Mikutano, Mkurugenzi Mkuu wa Uandishi wa Hotuba ya Mikutano Mkuu wa taarifa katika kitengo cha Dijitali.

Nyadhfa hizo zilikuwa zinashikiliwa na Dennis James Kinyua, Erick Ng'eno, David Nzioka na John Ndolo.

Licha ya kuwa Itumbi alikuwa akifanya kazi katika Ikulu mara nyingi amenukuliwa akiwakosoa vikali maafisa wakuu serikalini wakiwamo Mawaziri hasa kupitia mitandao ya Kijamii.

Si Mawaziri tu Itumbi amekuwa aikiikosoa vikali Idara ya Upelelzi DCI akimshtumu kwa kujikanganya kuhusu kesi kadhaa hasa za ufisadi.

Katika mtandao wake wa twita, Itumbi tayari amebadilisha  maelezo yake akisema yeye sasa ni mfugaji nguruwe. Itumbi amekuwa akiwafuga nguruwe kwa muda japo sasa huenda ikawa ndio riziki ya pekee kwa mujibu wa maelezo yake.