array(0) { } Radio Maisha | Masomo kuendele, japo nyumbani
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Masomo kuendele, japo nyumbani

Masomo kuendele, japo nyumbani

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Licha ya shule za msingi na upili kufungwa kufuatia maambukizi ya virusi vya korona, Wizara ya Elimu imeendeleza mikakati ya kuhakikisha wanafunzi hao wanaendelea na masomo wakiwa nyumbani kunzia Jumatatu wiki ijayo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu taasisi ya ukuzaji mtalaa, masomo yatendelea kupitia Redio ya Taifa- Idhaa ya Kingereza na Kiswahili kuanzia asubuhi  na kupeperushwa kupitia redio nyingine kadhaa sasa  ili kuwafikia wakazi wa eneo la Kaskazini Mashariki ya Kenya.

Pia masomo yataendelezwa kupitia runinga kutumia kituo cha Edu Channel ambacho pia kitapatika kupitia wavuti www.kicd.co.ke. Pia, baadhi ya  vitabu vitapatikana kupitia mfumo wa kieletroniki wa KICD- Kenya Education Cloud www.kec.ac.ke.

Waziri wa Elimu, Prof George  Magoha amewashauri walimu na wazazi kushirikiana ili kukabili athari za maambukizi ya virusi kwa sekta elimu ikizingatiwa virusi hivyo vimeanza kusambaa wakati ambapo shule nyingi  za msingi na upili zilikuwa mbioni kumaliza mtalaa na kuanza kuwandaa watahiniwa ili kufanya mitihani ya kitaifa baadaye mwaka huu.