array(0) { } Radio Maisha | Visa vya maambukizi ya korona duniani vyaongezeka
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Visa vya maambukizi ya korona duniani vyaongezeka

Visa vya maambukizi ya korona duniani vyaongezeka

Na Mike Nyagwoka,

NAIROBI, KENYA, Huku maambukizi ya Virusi vya Korona yakiendelea kusaambaa kote duniani, maafisa chini Uchina wamesema hakuna maambukizi yanayowahusisha wakazi wa miji wa Wuhan na Hubei japo watu kutoka maeneo mengine.

Wizara ya Afya nchini humo imesema katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita jumla ya maambukizi ya watu thelathini na wanne ni watu walioingia Uchina kutoka mataifa mengine. Aidha, ni watu wanane walioripotiwa kufariki dunia kutokana na virusi hivyo.
 
Jumla ya watu elfu themanini mia tisa ishirini na wanane wameambukizwa na wengine elfu tatu mia mbili arubaini na wawili wameaga dunia kutokana na korona.

Hayo yanajiri huku taifa la Italia likiripoti kufariki dunia kwa jumla ya watu mia nne sabini na watano katika kipindi cha saa ishirini na nne pekee, idadi kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa.

Nchini Korea Kusini watu 152 wameambukizwa hivi punde zaidi ikiwa idadi ya juu zaidi ya mabukizi chini ya kipindi cha siku moja. Barani Afrika idadai ya walioag dunia imefika 10 huku visa takriban 500 vikiripotiwa.

Jumatano, mtu wa kwanza kuaga dunia Kusini mwa Jangwa la Sahara aliaga dunia nchini Burkina Faso. Mwanamke mwenye uymri wa 62 na ambaye nia faisa wa ngazi ya juu katika bunge la taifa hilo aliaga dunia jana huku ikiarifiwa alikuwa pia akiugua kisukari kabla ya kuambukizwa virusi vya Korona.

Barani Afrika Shirika la Afya Duniani WHO liemonya kwamba huenda kuna maambukizi  zaidi ya inavyoripotiwa  ikizingatiwa kwamba mataifa mengi hayana vifaa vya kuwafanyia ukaguzi wanaoshukiwa kuugua.

Aidha, WHO imesema huenda hali ikawa mbaya zaidi iwapo mikakati haitaimarishwa zaidi ikizingatiwa maambukizi yameanza kuongezeka hasa katika taifa la Afrika Kusini ambalo sasa lina jumla ya watu mia moja kumi na sita ambao wameambukiwa. Tedros Adhanom Ghebreyesus ni Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

Kulingana na WHO jumla ya watu elfu nane mia tisa hamsini na tatu wamefarki dunia huku wengine elfu mia mbili kuni na tisa, na kumi na sita wakiugua.