array(0) { } Radio Maisha | Serikali yashinikizwa kutoa maelezo kuhusu virusi vya korona

Serikali yashinikizwa kutoa maelezo kuhusu virusi vya korona

Serikali yashinikizwa kutoa maelezo kuhusu virusi vya korona

Na Mike Nyagwoka,

NAIROBI, KENYA, Mahakama Kuu Alhamisi inatarajiwa kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Chama cha Mawakili, LSK kuitaka serikali ishinikizwe kutoa maelezo kuhusu mipango iliyoweza kuyakabili maambukizi ya Virusi vya Korona.

Agizo la kesi hiyo kusikilizwa lilitolewa Jumatatu wiki hii baada ya LSK kuandika barua ikitaka kesi hiyo kusikilizwa haraka iwzekanavyo. Ikumbukwe Tayari Idara ya Mahakama imetangaza mikakati iliyoweka kuhakikisha shughuli zinaendelea licha ya kusmabaa kwa virusi hivyo humu nchini.

LSK imesema licha ya serikali kutangaza kila siku kuhusu mipango yake haijatoa suluhu ya kudumu kuonesha wkmaba huduma muhimu hazitaathirika kufuatia Virusi hivyo.

Ikumbukwe awali mahakama ilitoa agizo kwa serikali kuweka wazi mipango yake ya kukabili janga hilo ambalo limeyaathiri zaidi ya mataifa mia moja kote duniani.

Aidha, mahakama iliishtumu serikali kufuatia hatua yake ya kuiruhusu ndege ya Uchina iliyokuwa na jumla ya abiria mia mbili thelathini na tisa kuwasili nchini, licha ya hali kuwa mbaya nchini humo. Licha ya agizo la mahakama iyo hiyo kwa serikali kuwatafuta na kuwaweka karantini abiria hao wote haijatoa taarifa zozote kuwahusu.