array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya maambukizi ya Korona yafika nne nchini Kenya

Idadi ya maambukizi ya Korona yafika nne nchini Kenya

Idadi ya maambukizi ya Korona yafika nne nchini Kenya

Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa Virusi vya Korona imefika wanne baada ya kisa kingine kuthibitishwa leo hii.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema aliyeambukizwa ni mtu aliyeingia nchini tarehe 9 mwezi huu kutoka London, Uingereza huku juhudi za kuwatambua waliotangamana naye zikiendelea.

Kagwe aidha amesema kufikia sasa watu 111 wamepimwa ili kubaini iwapo wameambukizwa tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza. Amesema wale ambao walibainika kutougua waliruhusiwa kwenda nyumbani.

Hata hivyo ili kuunusuru uchumi kutokana na madhara yanayotokana na Korona, serikali imeruhusu kuendelea kwa safari za ndege za mizigo huku wahudumu katika ndege hizo wakihitajika fanyiwa ukaguzi wa kina.