array(0) { } Radio Maisha | Tume ya Kutetea Haki za Binadamu inataka Korona kutangazwa janga la kitaifa

Tume ya Kutetea Haki za Binadamu inataka Korona kutangazwa janga la kitaifa

Tume ya Kutetea Haki za Binadamu inataka Korona kutangazwa janga la kitaifa

Tume ya Kutetea Haki za Binadamu, KHRC imetoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kulitangaza suala la Virusi vya Korona kuwa Janga la Kitaifa.

Katika taarifa kupitia Mkurugenzi Mkuu, George Kegoro, KHRC imesema Rais Kenyatta ana mamlaka ya kikatiba kutangaza Janga la Kitaifa endapo kuna shuhudiwa vita, majanga yasiyo ya kawaida ama iwapo kuna suala la dharura kuu nchini.

Kwa mujibu wa Katiba, kipindi cha dharura hudumu kwa siku 14 japo KHRC imesema kipindi hicho kinaweza kuongezwa hadi miezi miwili.

Tume hiyo imesema kutangazwa kwa hali ya dharura kutatoa fursa ya kushughulikiwa kwa kina kuhusu suala la Korona.

Aidha imesema hatua hiyo itasaidia kusitisha migawanyiko ya kisiasa ambayo imekuwa ikishuhudiwa huku Wakenya wote wakiwa na lengo moja la kukabili virusi hibyo.

KHRC hata hibyo imetangaza kuunga mkono mikakati iliyotangazwa na Rais Kenyatta ya kuzuia maambukizi kukiwamo kusitisha safari za ndege kutoka kwenye mataifa yaliyoathirika pakubwa.

Tayari Afrika Kusini imetangaza maambukizi ya Korona kuwa janga la kitaifa.