array(0) { } Radio Maisha | Mwanamume atengwa Mukuru akishukiwa kuwa na Korona

Mwanamume atengwa Mukuru akishukiwa kuwa na Korona

Mwanamume atengwa Mukuru akishukiwa kuwa na Korona

Mhudumu mmoja wa teksi ametengwa katika Hospitali ya Mukuru Health Centre baada ya kufika huko akihofia kuwa na maambukizi ya Virusi vya Korona.

Kwa mujibu wa Mwakilishi Wadi ya Imara, Kennedy Obuya, mhudumu huyo ambaye si mwenyeji wa eneo hilo alilazimika kutafuta huduma za matibabu katika kituo hicho baada ya kuwa na joto jingi  usiku wa kuamkia leo mwilini huku akihisi uchungu kifuani. Mwakilishi huyo amesema mtu huyo ni mhudumu wa texi  katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa JKIA.

Aidha amesema serikali ya Kaunti ya Nairobi imewatuma maafisa wa afya katika eneo hilo ili kufanikisha kuhamishwa kwa mtu huyo hadi hospitali zinazowahudumia watu waoshukiwa kuathiriwa.

 Hata hivyo amewataka wakazi kutohofu akisema wagonjwa ambao walikuwa wamekwenda kutafuta huduma katika hospitali hiyo wameelekwezwa kutafuta huduma kwingine.