array(0) { } Radio Maisha | Mwanamume atengwa Kericho baada ya kuonesha dalili zinazofanana na za Korona

Mwanamume atengwa Kericho baada ya kuonesha dalili zinazofanana na za Korona

Mwanamume atengwa Kericho baada ya kuonesha dalili zinazofanana na za Korona

Mwanamume anayeshukiwa kuwa na Virusi vya Korona anaendelea kutengwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Londiani kwenye Kaunti ya Kericho. Inaarifiwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 47 alipelekwa katika hospitali hiyo kufuatia dalili za kukohoa na kuumwa na viungo.

Mwanamume huyo ambaye ni mhubiri wa kidini alikuwa amerejea nyumbani kwake katika Kaunti ya Kericho baada ya kuhudhuria mkutano jijini Mombasa. 

Kisa hicho kiliripotiwa kwa maafisa wa afya siku ya Jumamosi japo kiliwekwa wazi jana jioni huku sampuli za mtu huyo zikichukuliwa kwa uchunguzi. Gavana wa kaunti hiyo, Paul Chepkony na afisa wa Huduma za Matibabu katika kaunti hiyo, David Ekuwam wamethibitisha kupata taarifa kuhusu kisa hicho.