array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa zaidi wa sakata ya utoaji tenda ghushi ya silaha wanaswa

Washukiwa zaidi wa sakata ya utoaji tenda ghushi ya silaha wanaswa

Washukiwa zaidi wa sakata ya utoaji tenda ghushi ya silaha wanaswa

Na Caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Washukiwa wawili zaidi wa sakata ya utoaji tenda gushi ya ununuzi wa vifaa vya kijeshi wanaendelea kuzuiliwa.

Wawili hao, Chrispine Oduor Oipo na Doreen Naomi Ratemo walikamatwa Jumatano jioni na maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI kwa kuaminika kuwa wakurugenzi wa kampuni ya Pzel Company Limited ambayo imehusishwa pakubwa katika sakata hiyo.

Wawili hao walipelekwa hadi katika makao makuu ya DCI kuhojiwa huku maafisa wa idara hiyo wakizikagua stakabadhi muhimu za kampuni hiyo ili kusaidia katika uchunguzi.

Haya yanajiri huku Niabu wa Rais William Ruto akifanya kila awezalo kujiondolea lawama kufuatia sakata hiyo ambayo imeipaka tope ofisi yake. Aidha inaarifiwa Niabu huyo wa Rais jana jioni alifanya mkutano na wafanyakazi katika ofisi yake, iliyoko katika jumba la Harambee na pia nyumbani kwake katika mtaa wa Karen.

Hapo jana  Ruto alidai kwamba tuhuma hizo ni ishara ya kudorora kwa usalama wake na wa ofisi yake. Katika barua iliyoandikwa na Mkuu wa Wafanyakazi katika ofisi yake Ken Osinde, Ruto sasa amemjukumu Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutywambai  na kibarua cha kutoa maelelezo ya watu walioandamana na Echesa alipotembelea ofisi hiyo.

Katika barua hiyo Osinde amemtaka Mutyambai kuanza kuwatambua watu waliondamana na Echesa kuingia katika ofisi yake Februari 13  na maafisa wa usalama waliowaruhusu kuingia.

Osinde pia amemtaka Mutyambai kuchunguza raia wa kigeni wanaodaiwa kuwa miongoni mwao na kubaini walivyoingia nchini na lengo lao. Kupitia Wizara ya Masuala ya Kigeni, Mutyambai ametakiwa pia kuweka wazi kampuni wanazohusishwa nazo na iwapo wana rekodi yoyote ya uhalifu.

Kufikia sasa wafanyakazi saba katika ofisi yake tayari wamehojiwa huku DCI ikishinikiza kupewa kamera zote za CCTV za ofisi ya Ruto kufanikisha uchunguzi