array(0) { } Radio Maisha | Abiria waliojificha baada ya kuvamiwa hawajulikani waliko

Abiria waliojificha baada ya kuvamiwa hawajulikani waliko

Abiria waliojificha baada ya kuvamiwa hawajulikani waliko

Na caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Abiria wengine waliokuwa wakisafiri katika basi ambalo lilishambuliwa jana na washukiwa wa Kundi gaidi la Al Shabaab kwenye Kaunti ya Mandera hawajulikani walipo baada ya kukimbilia usalama wao.

Abiria watatu walipigwa risasi na kufariki dunia, huku wengine wakifanikiwa utoroka.

Ripoti ya polisi inasema kuwa magaidi sita wa Al Shabaab waliokuwa wakitumia pikipiki, walilifyatulia risasi basi ambalo lilikuwa likija Nairobi na kuwaua abiria watatu na kuwajeruhi wengine watatu wanaotibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mandera.

Shambulio hilo la Jumatano lilijiri huku Waziri wa Elimu Profesa George Magoha na Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai wakitarajiwa kufika mbele ya Kamati ya Elimu Bungeni leo hii kuelezea sababu ya walimu kuendelea kuhama Kaskazini Mashariki kufuatia utovu wa usalama.

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi aliwaagiza viongozi hao kufika bungeni kutoa mwanga zaidi kuhusu suala hilo.

Agizo la Muturi linafuatia malalamiko kutoka kwa viongozi wa Kaskazini Mashariki wakiongozwa na Mbunge wa Wajir Magharibi Ahmed Kolosh ambao wamelalamikia kukwama kwa shughuli za masomo kufuatia uhamisho huo.

Takriban walimu elfu moja wasiokuwa wazaliwa wa Kaskazini Mashariki wamehama kutoka eneo hilo kufuatia mashambulio yanayotelezwa na Al Shabaab.

Magaidi hao wamekuwa wakiwalenga walimu wasiokuwa wa Kaskazini Mashariki hatua ambayo imewaskuma walimu hao kuiomba Tume ya Huduma za Walimu TSC kuwapa uhamisho.

Mapema wiki hii Matiang'i aliwahakikishia viongozi wa Kaunti za Wajir, Garissa na Mandera kwamba serikali itashughulikia suala la utovu wa usalama.Wanafunzi takriban elfu tatu wa kaunti hizo kwa sasa wanataabika kupata elimu kufuatia uhamisho huo.

Katika vikao vya Jumatano, Maseneta walijadili suala hilo huku wakitoa wito kwa Serikali Kuu kulishughulikia tatizo hilo haraka iwezekanavyo.