array(0) { } Radio Maisha | Echesa aliingiaje katika ofisi yangu-Ruto amuuliza Mutymbai

Echesa aliingiaje katika ofisi yangu-Ruto amuuliza Mutymbai

Echesa aliingiaje katika ofisi yangu-Ruto amuuliza Mutymbai

Uchunguzi wa sakata ya ulagahai dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Michezo  Rashid Echesa  umechukua  mkondo mpya baada ya Naibu wa Rais William Ruto kudai  tuhuma hizo ni ishara ya kudorora kwa usalama wake na wa ofisi yake. Kufuatia barua iliyoandikwa  na Mkuu wa Wafanyakazi katika ofisi yake Ken Osinde, Ruto sasa amemjukumu Inspekta Mkuu wa Polisi na kibarua cha kutoa maelelezo ya watu walioandamana na Echesa alipotembelea ofisi hiyo. Osinde amemtaka Hillary Muityambia kuanza  kwa kuwatambua watu waliondamana na Echesa kuingia katia ofisi yake tarehe 13 mwezi Februari na maafisa wa usalama waliowaruhusu kuingia.

Osinde pia amemtaka Mutyambai kuchunguza raia wa kigeni wanaodaiwa kuwa miongoni mwao na kubaini walivyoingia nchini na lengo lao la kuingia nchini. Kupitia Wizara ya Masuala ya Kigeni, Mutyambai ametakiwa pia kuweka wazi kampuni wanazohusishwa nazo na iwapo wana rekodi yoyote ya uhalifu.

Ikumbukwe raia wa kigeni ambao wametajwa kuwa wawakilishi wa Kampuni ya Eco Advanced Technologies ni Stanley Kozlowski ambaye ni raia wa Marekani na raia wa Misri Mamdouh Mostafa Amer Lofty huku Wakenya waliohusika na hata kufikishwa  mahakamani mbali na Echesa wakiwa ni   Daniel Otieno, Clifford Okoth and Kennedy Oyoo. 

Raia hao  wawili hao walidai kuingia katika ofisi ya Ruto mara mbili kadhalika kuingia katika ofisi za Wizara ya Ulinzi huku wakisindikizwa na magari ya kifahari yaliyowapa imani kwamba walikuwa mikononi pa maafisa halisi wa serikali. Hata hivyo, Wizara ya Ulinzi imepinga taarifa hiyo na kusema hawakuwahi kufika wala kutangamana na maafisa wa Wizara ya Ulinzi

Ruto kupitia Osinde ametaka kampuni hiyo pia kuchunguzwa ili kubaini iwapo  ina uwezo wa kutekeleza  zabuni ya  silaha za kijeshi kiasi cha shilingi bilioni 39.5 inavyodaiwa katika kesi dhidi ya Echesa na mwishowe kutanga Mutyambai kuweka wazi hatua zitakazochukuliwa ili kuzuia hali sawa na hiyo kurejelewa.

Baadhi ya mashtaka yanayowakabili ni ya kughushi stakabadhi , kupokea fedha kutumia uwongo na kupanga kutejeleza uhalifu- mashtaka ambayo waliyakana kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.

Tayari maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wamewahoji baadhi ya wafanyakazi katika ofisi ya Naibu wa Rais huku wafanyakazi wengine zaidi wakitarajiwa kuhojiwa.