array(0) { } Radio Maisha | Matiang'i apata pigo maakamani

Matiang'i apata pigo maakamani

Matiang'i apata pigo maakamani

Waziri wa Masuala ya Ndani Dakta-Fred Matiang'i amepata pigo baada ya Mahakama Kuu kubatilisha agizo alilotowa la kuwarejesha makwao raia wanne wa Uchina.

Jaji wa Mahakama Kuu Luka Kimaru amepinga uamuzi wa Matiang'i akisema kuwa raia hao wamo katika hatari ya kukumbwa na Virusi vya Corona ambavyo vimesambaa katika taifa lao.

Matiangi alitoa agizo hilo Februari 13 baada ya mmoja wao kunaswa katika kanda ya video akimcharaza mfanyakazi wake kwa madai ya kuchelewa kazini.

Kimaru aidha amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP, Nordin Haji kuwasilisha ombi kuhusu suala hilo Februari 25 akitaja suala hilo kuwa la dharura.

Mahakama aidha, imekataa kuendelea kuzuiliwa washukiwa kwa siku ishirini na moja na kusema kuwa watazuiliwa kwa siku kumi na tano pekee.

Matiang' alitekeleza uamuzi huo baada ya kubainika kwamba mshukiwa hakuwa na kibali cha kufanya kazi humu nchini licha ya kuwa mmiliki wa mkahawa mmoja katika mtaa wa Kileleshwa hapa jijini Nairobi.