array(0) { } Radio Maisha | Noordin Hajj aapa kukabili ufisadi katika Bandari ya Mombasa

Noordin Hajj aapa kukabili ufisadi katika Bandari ya Mombasa

Noordin Hajj aapa kukabili ufisadi katika Bandari ya Mombasa

Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji amesema ofisi yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali inaposhughulikia kesi za ufisadi katika Bandari ya Mombasa.

Haji amesema kwamba hali hiyo imechangia pakubwa kukithiri kwa uingizaji wa bidhaa gushi nchini kupitia bandari hiyo.

Akihutubu wakati wa kongamano kuhusu mikakati ya uingizaji na usafirishaji wa mizigo jijini Mombasa, Haji amesema kwamba moja wapo ya changamoto hizo ni ukosefu wa stakabadhi za uangizaji wa mizigo nchini.

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Matiang'i amesema tatizo kuu ni kuhusu kuingizwa kwa dawa gusgi na silaha aharamu kupitia mbadari hiyo ya Mombasa. Matiang'i amesema licha ya serikali kuimarisha mikakati tatizo la silaha aharamu limeendelea kushuhudiwa nchini.

Waziri huyo amesema katika kipindi cha miezi miwili ijayo serikali inapanga kuteketeza kati  ya silaha elfu tano na sita haramu ambazo zimeingizwa nchini kinyume na sheria.

Maafisa wengine wakuu serikalini wanaohudhuria kongamano hilo ni Gavana wa Benki Kuu CBK, Patrick Njoroge, Mkurugenzi wa Mamalka ya Kitaifa ya Kukabili bidhaa Gushi Elema Halake ni miongoni mwa wanaohudhuria kongamano hilo.