array(0) { } Radio Maisha | Raia wa Uchina atengwa Nakuru akionesha dalili za Corona

Raia wa Uchina atengwa Nakuru akionesha dalili za Corona

Raia wa Uchina atengwa Nakuru akionesha dalili za Corona

Raia wa Uchina aliyewasili nchini Jumapili iliyopita kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta angali ametengwa na umma katika nyumba yake mjini Nakuru baada ya kuonesha dalili za ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Inaarifiwa kwamba raia huyo aliwasili nchini Jumapili na kupanda texi kutoka JKIA hadi mtaani Upper Hill kwenye Kaunti ya Nakuru na kwamba alikuwa akilalamikia maumivu kwenye viungo vya mwili pamoja na joto jingi mwilini.

Hata hivyo, Wizara ya Afya imewataka wananchi kutokuwa na hofu na kusisitiza kwamba i tayari kuvidhibiti virusi hivyo.