array(0) { } Radio Maisha | KPA yalaumiwa kwa kuongeza ada ya kukagua mizigo

KPA yalaumiwa kwa kuongeza ada ya kukagua mizigo

KPA yalaumiwa kwa kuongeza ada ya kukagua mizigo

Mawakala wa Kampuni za kukagua mizigo katika Bandari ya Nchi Kavu, eneo la Embakasi hapa Jijini Nairobi, wamendamana wakiilamu Mamlaka ya Bandari Nchini KPA kwa madai ya kuwanyanyasa.

Mawakala hao waliandamana hadi katika makao makuu ya Shirika la Habari la Standard Group PLC hapa Jijini Nairobi, na hata kusababisha msongamano wa magari kwenye Barabara Kuu ya Mombasa - Nairobi, wakitaka kilio chao kuangaziwa.

Mawakala hao wamedai usimamizi wa KPA umeongeza ada za kuigakua mizigo bila kuwahusisha.

Juhudi za kuzungumza na usimamizi wa KPA ili kupata ufafanuzi kuhusu madai haya hazikufaulu.