array(0) { } Radio Maisha | Mudavadi apendekeza kutobuniuwa kwa serikalai za kimaeneo

Mudavadi apendekeza kutobuniuwa kwa serikalai za kimaeneo

Mudavadi apendekeza kutobuniuwa kwa serikalai za kimaeneo

Kamati ya Uendeshaji ya Mpango wa Upatishi BBI siku ya Jumanne ilipokea maoni kuhusu ripoti ya BBI  kutoka kwa Kinara wa ANC Musalia Mudavadi na viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini katika jumba la KICC hapa jijini Niarobi.

Miongoni mwa mapendekezo ambayo Mudavadi aliwasilisha ni pamoja na kutobuniwa kwa serikali za kimaeneo, marekebisho katika Tume ya Uchaguzi IEBC. Aidha wanafuzi wa vyuo vikuu walipendekeza kudumishwa kwa usalama wao wanapokuwa shuleni.

Mudavavdi alisema kuwa anaunga kuwapo kwa wadhifa wa Waziri Mkuu na manaibu wake ila pana haja ya kuweka wazi majukumu ya Rais ,Waziri Mkuu na manaibu wake amabayo yatalindwa kikamilifu kikatiba, huku akipinga pendekezo la kubuniwa kwa serikali za kimaeneo.

Akizungimzia Tume ya uchaguzi IEBC, Mudavadi alipendekza Tume hiyo ikabidhiwe uhuru unaostahili, kwa kuhakikisha bajeti yake imejumuishwa kuwa miongoni mwa zile za idara huru badala ya kuitegemea serikali moja kwa moja. Vilevile alitaka IEBC Itekeleze majukumu yake vilivyo mfano uhamasisho wa wanachi kabla ya uchaguzi na ripoti kamili ya idadi ya wapiga kura, kura zilizopigwa na kura zilizoharibika.

Suala la amani na utangamano Mudavadi alisema kuwa ni muhimu kujumuisha jamii mbali mbali ikiwa njia ya kuboresha amani lakini muhimu zaidi ni kuhakikisha jamii zingine hazitengwi.

Akizungumzia suala la Uchumi, Mudavadi alipendekeza kuwepo kwa Mamlaka Huru itakayosismamia sekta ya madeni itakayo hamasisha umma kuhusu deni la taifa na mikakati inayowekwa kuilipa.Mudavadi amesema pana haja ya sera za uchumi kuangaziwa upya ili kuwapo kwa mazingira bora ya kibaishara na hivyo basi kuimarisha uchumi.
 
Mudavadi vilevile, alipendekeza kuwa  miongoni mwa mikakati inayoweza kuwekwa kukabili ufisadi ni kuhakikisha Tume ya Huduma za Mahakama JSC inafadhiliwa vilivyo, vilevile viongozi mbali mbali wafanyiwe ukaguzi na misingi ya mali yao iwekwe wazi.
 
Alipendekeza kufufuliwa kwa kampuni mbali mbali ikiwa njia ya kuboresha uchumi wa taifa. Miongoni mwa kampuni hizo ni Mumias, Nzoia,  Chemelil, Sony,na Muhoroni.

Mudavadi hata hivyo, alihofia mustakabali wa mchakato wa BBI akisema kuna mifano mingi ya michakato sawa na hiyo ambayo imefeli,  akiongeza kuwa tatizo kuu humu nchini limekuwa ni msukumo wa kisiasa katika kufanikisha mageuzi kupitia ripoti mbalimbali.

Katika kikao hicho viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini walisisitiza haja ya kutilia maanani suala la usalama wao wanapokuwa vyuoni. walipendekeza kila chuo kuwa na kituo cha polisi ambacho kitashughulikia usalama wao. Walipendekeza kuwepo kwa kamati huru itakayo jadili masuala ya nidhamu katika vyuo hivyo.

Kuhusu suala la Mkopo wa Kufadhili Elimu ya Juu, HELB  wanafunzi hao waliipongeza serikali kwa kuanzisha mpango huo huku wakisisitiza haja ya kuboreshwa hata zaidi ili kuwafikia wanafunzi wengi.

Aidha walipendekeza kuondolewa kwa kiwango cha riba kinachotozwa wanaochukua mkopo huo hasa ikizingatiwa kuwa wamekuwa wakitozwa kiwango cha riba cha asilimia nne.Wakati uo huo, wamependekeza kuondolewa kwa muda wanaotakiwa kulipa mkopo huo, kwa kuwa ni vigumu kwa wanaohitimu kupata kazi kwa haraka.

Wanafunzi hao walipendekeza baadhi yao wajumuishwe katika kamati hiyo, penedelkezo amablo amablao limetupiliwa mabli na wanakamati hao waliosema kuwa tayari vijana wamewailishwa. Aidha, walipendekeza kuwepo sheria itakayo hakikisha vijana wanajiunga na Shirika la Huduma kwa Vijana NYS kabla ya kujiunga na Vyuo Vikuu.