array(0) { } Radio Maisha | Kinara wa ANC, Musalia Mudavadi apinga pendekezo la serikali za kimaeneo

Kinara wa ANC, Musalia Mudavadi apinga pendekezo la serikali za kimaeneo

Kinara wa ANC, Musalia Mudavadi apinga pendekezo la serikali za kimaeneo
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi amepinga pendekezo la kubuni serikali za kimaeneo.
 
Akizungumza wakati wa kutoa mchango wake wakati wa vikao vya Kamati ya Kuendesha Shughuli za Mpango wa Upatanishi BBI, Jijini Nairobi, Mudavadi amesema hatua hiyo itaongeza mzigo kwa Mkenya mlipakodi.
 
Mudavadi amesisitiza kwamba Kenya haifai mfumo wa serikali tatu kwa pamoja ikizingatiwa sasa kuna serikali ya kitaifa na zile za kaunti.
 
Pendekezo la kubuni serikali za kimaeneo kwa kuzingatia mikoa minane ya awali, limekuwa likishinikizwa hasa na baadhi ya magavana ambao wanakamilisha muhula wao wa pili katika mkutano ya BBI.