array(0) { } Radio Maisha | Hakimu Mkuu alijiondoa katika kesi ya Babu Owino

Hakimu Mkuu alijiondoa katika kesi ya Babu Owino

Hakimu Mkuu alijiondoa katika kesi ya Babu Owino

Hakimu Mkuu Francis Andayi amejiondoa katika kesi ya mauaji inayomkabli Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino.

Akitetea uamuzi huo, Andayi amesema Mkurugenzi Mkuu wa Mashataka ya Umma DPP aliandika barua kwa Idara ya Mahakama akilalamikia jinsi alivyomwachilia Babu kwa dhamana, akiitaka mahakama kuangazia upya dhamana aliyopewa Babu Owino.

Andayi ambaye amekuwa akiisilikiza kesi hiyo, ambapo Babu Owino anadaiwa kumpiga risasi shingoni Mchezaji Santuri Dj Elvove katika Kilabu kimoja hapa jijini Nairobi, badala yake amelielekeza ombi la DPP kwa Hakimu Bernard Ochoi ambaye sasa ndiye atakayesikiliza kesi hiyo.

Aidha ombi hilo linatarajiwa kutajwa mahakamani mwezi Machi tareje mbili mwaka huu.

Mahakama ya Milimani ilimwachilia Babu Owino kwa dhamana ya shilingi milioni kumi, licha ya upande wa mlalamishi kudai kwamba maisha yao yatakuwa hatarini iwapo ataachiliwa.

abu Owino alishtakiwa mnamo tarehe kumi na saba mwezi Januari mwaka huu.