array(0) { } Radio Maisha | Mamlaka ya IPOA yagatua utendaakazi wake kuwafikia wananchi

Mamlaka ya IPOA yagatua utendaakazi wake kuwafikia wananchi

Mamlaka ya IPOA yagatua utendaakazi wake kuwafikia wananchi

Mamlaka ya Kutathmini Utendakazi wa Polisi IPOA, imeanzisha mpango wa kugatua utendakazi wake hadi mashinani ikiwa njia mojawapo ya kuwafikia Wakenya wote na kufuatilia kwa karibu shughuli za polisi.

IPOA imesema wakati umefika wa kuwahusisha Wakenya kwa karibu ili kuimarisha utendakazi wake.

Mwenyekiti wa IPOA Ann Makori amesema kuwa mamlaka hiyo imeweka kipau mbele malalamiko ya raia huku akisema kuwa itaendelea kuwalinda wanaopeleka malalamiko kuhusu vifo vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi.

Akizungumza wakati wa mkutono wa kutoa kwa ripoti ya mwaka wa 2019 kuhusu mauaji ya raia yaliotekelezwa na maafisa wa polisi, Makori amewahakikishia wananchi kwamba maafisa waliohusika katika mauaji watajkabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Vuilevile, Makori amesema IPOA ina uwezo wa kuingilia kati kesi ambazo zinacheleweshwa na Idara ya Polisi ili kuhakikisha haki inapatikana kwa familia za waliouliwa.