array(0) { } Radio Maisha | Waziri wa Elimu Prof. Magoha aagiza kufungwa kwa baadhi ya vyuo

Waziri wa Elimu Prof. Magoha aagiza kufungwa kwa baadhi ya vyuo

Waziri wa Elimu Prof. Magoha aagiza kufungwa kwa baadhi ya vyuo

Wizara ya Elimu imeagiza kufungwa kwa baadhi ya vyuo vikuu na kujumuishwa kwa mabewa mbalimbali ikiwa njia mojawapo ya kuboresha viwango vya elimu nchini.

Wiziri wa Elimu Prof. George Magoha amesema kuchipuka kwa vyuo vingi nchini kumechangia pakubwa kushuka kwa viwango vya elimu huku akiagiza kufungwa kwa vyuo ambavyo havijaafikia viwango vinavyohitajika.

Akizungumza wakati wa mkutano na Manaibu Wakuu wa Vyuo, Magoha ameagiza kutoanzishwa kwa vyuo zaidi akisema baadhi ya vyuo hivyo havina miundo msingi bora huku wazazi wakiendelea kupunjwa na usimamizi.

Haya yanajiri huku washikadau katika sekta ya elimu wakiendelea kulalamikia kushuka kwa viwango vya elimu kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanajiunga na vyuo vikuu.