array(0) { } Radio Maisha | Rashid Echesa na washukiwa wenza waachiliwa kwa dhamana

Rashid Echesa na washukiwa wenza waachiliwa kwa dhamana

Rashid Echesa na washukiwa wenza waachiliwa kwa dhamana

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa na washtakiwa wenza watatu wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni tatu kila mmoja.

Wanne hao akiwamo Echesa, Daniel Otieno, Clifford Okoth Onyango na Kennedy Oyoo wamefikishwa katika Mahakama ya Milimani wakikabiliwa na mashtaka sita likiwamo kujaribu kughushi stakabadhi ili kufanikisha ununuzi wa vifaa vya kivita.

Wakiwa mbele ya Hakimu Mkuu Kennedy Cheruiyot, Echesa na wenzake wamekana mashtaka yote dhidi yao baada ya kusomewa mashtaka kumi na mawili katika sakata hiyo ya thamani ya shilingi bilioni 39.5

Katika kikao cha leo upande w utetezi ukiongozwa na umeibua madai kwamba Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ODPP imekosa kuheshimu maagizo ya mahakama baada ya kufanya uchunguzi nyumbani kwa Echesa Jumamosi badala ya Jumatatu jinsi ilivyoagiza mahakama.

Echesa aidha amekana madai ya kujifanya kuwa Msaidizi wa Naibu wa Rais William Ruto.

Aidha upande wa mashtaka ulikuwa umeiomba mahakama kutowaachilia wanne hao kwa kuwa huenda wakahitilafiana na uchunguzi, hoja ambayo imepuuzwa na upande wa utetezi.

Ikumbukwe hii ni mara ya pili kwa washukiwa hawa kupewa dhamana hiyo, baada ya awali kupewa dhamana iyo hiyo na Mahakama ya JKIA.

Kukamatwa kwa Echesa aidha kuliibua mjadala mkali miongoni mwa viongozi wa kisiasa hasa baada ya Ofisi ya Naibu wa Rais William Ruto kuhusishwa na sakata hiyo, baada ya kukiri kwamba Echesa na wenzake walifanya mkutano ofisini mwake kwa muda wa dakika 23.

Gavana wa Kitui Charity Ngilu, Seneta wa Siaya James Orengo vilevile aliyekuwa Mbunge wa Kibwezi Kalembe Ndile walimtaka Naibu wa Rais William Ruto kuzungumza kuhusu anayoyafahamu kuhusu sakata hiyo au ajiuzulu