array(0) { } Radio Maisha | Maafisa wa DCI wafanya uchunguzi ofisini kwa Naibu wa Rais William Ruto katika Jumbe la Harambee Annex

Maafisa wa DCI wafanya uchunguzi ofisini kwa Naibu wa Rais William Ruto katika Jumbe la Harambee Annex

Maafisa wa DCI wafanya uchunguzi ofisini kwa Naibu wa Rais William Ruto katika Jumbe la Harambee Annex

Makachero wa Idara ya Upelelezi DCI wamefanya uchunguzi katika Ofisi ya Naibu wa Rais William Ruto katika Jumba la Harambee Annex siku moja tu baada ya Ruto kukiri kwamba aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa na washukiwa wenza katika sakata ya zabuni bandia ya vifaa vya kivita, waliitembelea ofisi hiyo.

Inaarifiwa kwamba maafisa hao wamewahoji wafanyakazi katika ofisi hiyo huku wakizikagua kamera za CCTV kwa umakini.

Echesa na washukiwa wengine watatu katika sakata hiyo akiwamo Daniel Otieno, Clifford Okoth Onyango, na Kennedy Oyoo wamefikishwa katika Mahakama ya Milimani na kukabiliwa na mashtaka kadhaa likiwamo lile la kugushi stakabadhi ili kutekeleza biashara hiyo.

Wanne hao walikamatwa na kufikishwa mahakamani kufuatia sakata hiyo ambayo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 39.5.

Aidha katika ujumbe wake kwenye mtandao wa twitter alizitaka idara za uchunguzi kuichunguza Idara ya Ulinzi, akisema kuwa ununuzi wa vifaa vya ulinzi hauwezi kufanywa pasi kuidhinishwa na idara hiyo.

Tayari viongozi mbalimbali akiwamo Gavana wa Kitui Charity Ngilu, Seneta wa Siaya James Orengo vilevile aliyekuwa Mbunge wa Kibwezi Kalembe Ndile wamemtaka Naibu wa Rais William Ruto kutoa taarifa kamili ya anayoyajua kuhusu sakata hiyo, la sivyo ajiuzulu.