array(0) { } Radio Maisha | Raila azungumzia kuachiliwa kwa Jowie Irungu baada ya kuimba Jowi mara tatu katika mazishi ya Hayati Moi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Raila azungumzia kuachiliwa kwa Jowie Irungu baada ya kuimba Jowi mara tatu katika mazishi ya Hayati Moi

Raila azungumzia kuachiliwa kwa Jowie Irungu baada ya kuimba Jowi mara tatu katika mazishi ya Hayati Moi

Kinara wa ODM Raila Odinga amekuwa mgeni wa heshima katika hafla ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shule ya Upili ya Wavulana ya Maranda siku ya Ijumaa.

Odinga ameeleza historia fupi ya Shule hiyo, akisema kabla iwe shule sehemu hiyo ilitumiwa kuwa mahali pa burudani wa watu kuvinjari wakiwa wamevaa ngozi za wanyama na densi za kiafrika. Odinga vilevile ameeleza umuhimu wa elimu bora na kutoa wito wa kuwapa vijana ujuzi ili wanapomaliza shule wanaweza kujikimu kimaisha bila kutegemea ajira. Aidha, Raila kwa mara nyingine ametumia fursa hiyo kuwasuta viongozi wa kisiasa wanaotoa fedha nyingi makanisani kwa ajili ya michango.

Odinga ametumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa Jaji Mkuu David Maraga kuhakikisha kesi zinaskizwa kwa wakati ufaao na uamuzi kupatikana ili watu fisadi wapate funzo na wanaokandamizwa wapate haki. Odinga ametaja kuachiliwa kwa mshukiwa mkuu wa kesi ya mfanyabiashara Monica Kimani, Joseph Irungu maarufu Jowi akichekesha umati kuwa baada ya kuimba katika matanga ya Hayati Daniel Moi na kutaja Jowi Jowi mara tatu  Jowie hatimaye aliachiliwa keshoye.

Maraga ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule hiyo amesema kuwa Shule ya Maranda ilikuwa msingi bora maishani mwake akisistiza umuhimu wa elimu.

Seneta wa Siaya James Orengo vilevile amejiunga na viongoz wengine kuisifu  Maranda kwa kuwa moja wapo ya shule ambazo zimekuwa na viongozi tajika nchini, akitumia mfano wa kesi iliyowasilishwa na Kinara wa ODM Raila Odinga kupinga uchaguzi wa mwaka 2017, akiwachekesha wengi kwa kusema kuwa aliyewasilisha kesia Odinga alikuwa mwanfunzi wa randa, wakili wake Otiende Omollo alikuwa mwanafunzi wa Marnda vilevile jaji Mkuu David Maraga alikuwa mwanafunzi wa Maranda.