×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Magoha: Asilimia 100 ya wanafunzi wamejiunga na shule za upili katika maeneo ya Nyanza,Magharibi, Kaskazi Mashariki mwa Nchi na maeneo ya kati

Magoha: Asilimia 100 ya wanafunzi wamejiunga na shule za upili katika maeneo ya Nyanza,Magharibi, Kaskazi Mashariki mwa Nchi na maeneo ya kati

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha amesema kuwa maeneo ya Nyanza, Magharibi ya Nchi maeneo ya Kati na Kaskazini Mashariki yamekuwa na asilimia 100 ya idadi ya wanafunzi waliojiunga na shule za upili, huku maeneo mengine yakiwa na kati ya asilimia 98 na 99. Akizungumza siku ya Ijumaa wakati wa maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa shule ya Upili ya Wavulana ya Maranda, Magoha amesema kuwa kwa jumla idadi kamili ya waliojiunga na shule za upili ni asilimia 99.5.  

Vilevile Magoja ametoa wito kwa viongozi wote tajika waliosomea katika shule hiyo kujikakamua kuboresha miundo msingi shuleni humo bila kusubiri serikali iboreshe shule hiyo.

Katika hafla hiyo, Seneta wa Siaya James Orengo amejiunga na viongozi wengine kuisifu shule ya  Maranda kwa kuwa mojawapo ya shule ambazo zimekuwa na viongozi tajika nchini, akitumia mfano wa kesi iliyowasilishwa na Kinara wa ODM Raila Odinga kupinga uchaguzi wa mwaka 2017, akiwafurahisha wengi kwa kusema kuwa aliyewasilisha kesi ya Odinga, Wakili Otiende Omollo alikuwa mwanafunzi wa Maranda, vilevile Jaji Mkuu David Maraga.

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni wanafunzi wa zamani Kinara wa ODM  Raila Odinga, Jaji Mkuu David Maraga, na Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo.