array(0) { } Radio Maisha | Marais wa kigeni wahudhuria Ibada ya kitaifa ya Mzee Moi

Marais wa kigeni wahudhuria Ibada ya kitaifa ya Mzee Moi

Marais wa kigeni wahudhuria Ibada ya kitaifa ya Mzee Moi

Hayati Mzee Daniel Toroitich Arap Moi ametajwa kuwa Kigogo wa Kisiasa, nguzo kuu ya maendeleo, amani na ushirikiano baina ya Kenya na mataifa ya Jumuiya ya Afrika.

Marais wa mataifa zaidi ya matano ya Afrika wamesema kuwa Mzee Moi alichangia pakubwa kuimarika kwa miungano ya maendeleo ya Bara la Afrika yakiwamo EAC, IGAD na COMESA.

Wakizungumza wakati wa Ibada ya Kitaifa ya Mzee Moi katika Uwanja wa Nyayo hapa jijini Nairobi, marais hao wakiongozwa na Yoweri Museveni wa Uganda wamemmiminia sifa tele Hayati Moi wakimtaja kuwa kiongozi aliyeleta amani nchini na kwenye mataifa ya Afrika.

Museveni aidha amesema kuwa ushirikiano baina ya Kenya na Uganda umeendelea kuimarika kuanzia miaka ya awali hali ambayo imeboresha pakubwa biashara na maendeleo kutokana na uzalendo wa Moi na moyo wa maridhiano.

Marais wakiwamo aliyekuwa Rais wa tatu waTanzania Benjamin Mkapa aliyesoma risala za Rais John Magufuli, Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde, Salva Kiiri wa Sudan na Ishmail Omar wa Djibouti wamesema Moi alichangia zaidi kufufuliwa kwa Jumuia ya  Afrika Mashariki,  amani na ustawi baina ya Kenya na mataifa jirani.

Marais wengine waliohutubu katika hafla hiyo ni  Paul Kagame wa Rwanda, Rahim Gadhi Zaharawi Naibu wa Rais wa Nigeria miongoni mwa wengine. Sawa tu na wenzao wamemtaja Moi kuwa rafiki wa karibu wa mataifa yao.

Marais zaidi wa watano, wajumbe mbalimbali, mabalozi na wawakilishi wao wamehudhuria ibada hiyo ya kitaifa.