array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Kanisa la AIC waongoza Ibada ya Kitaifa ya Hayati Moi

Viongozi wa Kanisa la AIC waongoza Ibada ya Kitaifa ya Hayati Moi

Viongozi wa Kanisa la AIC waongoza Ibada ya Kitaifa ya Hayati Moi

Ibada ya Kitaifa ya mwenzadake Hayati Daniel Toroitich Arap Moi inaendelea katika Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi huku ikiongozwa na Kanisa la African Inland Church, AIC ambalo Moi alikuwa muumini wake.

Askofu Mstaafu wa kanisa hilo, Silas Yego ambaye amemfahamu Moi kwa miaka mingi, amepewa fursa ya kuhubiri wakati wa ibada hiyo huku mahubiri yake yakijikita katika vifungu mbalimbali vya Biblia ambavyo Moi alikuwa amevipenda.

Aidha, Yego ametumia fursa hiyo kuwarai viongozi kuiga mfano wa Moi katika kuhimiza amani nchini akisema Moi alijali sana amani na kuwataka kutotumia vyeo vyao kuliharibu taifa bali kulijenga.

Ibada hiyo imeendeshwa kwa utaratibu maalum huku pambio vilevile vifungu vya Biblia vikosomwa. Mwanawe Moi, Philip Moi ni miongoni mwa waliosoma vifungu vya Biblia wakati wa ibada.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali vilevile walipewa fursa katika ibada hiyo huku wakiongoza maombi kwa familia ya mwendazake Moi.

Utaratibu wa ibada hiyo ulianzia kwa uelekezi wa viongozi wa kiroho katika Jeshi la Ulinzi, KDF kisha maombi yaliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la AIC, Paul Kirui na kufuatiwa na pambio vilevile maandiko katika Biblia.

Viongozi wengine wa kidini waliohudhuria ibada hiyo ni Askofu Mkuu wa Kanisa Kianglikana nchi, Jackson Ole Sapit vilevile Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Kadinali, John Njue miongoni mwa wengine.