array(0) { } Radio Maisha | Maana ya jina Toroitich alilopewa Hayati Mzee Moi

Maana ya jina Toroitich alilopewa Hayati Mzee Moi

Maana ya jina Toroitich alilopewa Hayati Mzee Moi

Mwanawe Moi, Raymond Moi amesoma historia ya babaye ambapo ameelezea kwa kina mikakati hayati Moi aliyoweka katika sekta ya elimu kwa kuboresha mazingira ya walimu kwa kupigania kuwepo kwa Chama vyama vya kupigania haki za walimu Afrika.

Vilevile, Raymond amerejelea kauli iliyotolewa na wengi kwamba marehemu alilipa umbele suala la amani nchini na hata katika mataifa jirani ikiwemo Sudan Kusini.

Wakati uo huo, katika hotuba yake, Raymond amedokeza kwamba babaye alipewa jina Toroitich lililomaanisha 'Kukaribisha nyumbani Ng'ombe' . Moi alifunga ndoa na marehemu mkewe Lena mwaka wa 1950 na kubarikiwa na watoto wanane, watano wakiume na watatu wakike.