array(0) { } Radio Maisha | Wanasayansi waendeleza utafiti wa Chanjo dhidi ya HIV baada ya matokeo ya awali kutupiliwa mbali.
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wanasayansi waendeleza utafiti wa Chanjo dhidi ya HIV baada ya matokeo ya awali kutupiliwa mbali.

Wanasayansi waendeleza utafiti wa Chanjo dhidi ya HIV baada ya matokeo ya awali kutupiliwa mbali.

Wiki moja tangu shughuli ya kubaini uwezo wa chanjo dhidi ya virusi vya HIV HVTN  702  kusitishwa na kuwavunja moyo wengi waliodhania hatimaye mbinu mwafaka ya kuzuia maambukizi imebuniwa, wanasayansi na watafiti wa chanjo hiyo wamehakikisha kuwa bado kunamatumaini ya kubuni chanjo nyingine itakayosaidia pakubwa katika kuzuia maambukizi.

Chanjo hiyo ilisitishwa kwa misingi kuwa haijafikia viwango vya kuzuia maambukizi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa ya Chanjo dhidi ya Virusi vya HIV, Daktari Kundai Chenyenze, matumaini yapo kwani majaribio bado yanaendelea katika mataifa mbali mbali.

"Hatujafa moyo, kama watafiti tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha chanjo dhabiti inapatikana, tumejifunza mengi kutokana na utafiti huo na tutahakikisha tunabuni chanjo kamili na ya bei nafuu itakayopunguza maambukizi ya HIV."

Kauli sawa na hiyo ilitolewa na mmoja wa watafiti wakuu katika taasisi  ya IAVI Profesa Omu Anzala, amabaye amesisitizia umuhimu wa kupimwa na matumizi ya dawa ya PEP zinazozuia maambukizi.

Mjaribio ya chanjo hiyo ya HVTN  702  maarufu Uhambo trial  yalifanyika katika taifa la Afrika Kusini kunzia mwaka 2016 ambapo watu 5,407 walijitokeza kufanyiwa majaribio.

Watu hao waliochaguliwa walikuwa wakiume na wakike walio kati ya miaka 18 na 35, vilevile wanoshiriki ngono.

Daktari Chenyenze anaeleza kuwa baadhi ya waliofanyiwa majaribio waliambikizwa virusi hivyo sababu kuu iliyosababisha chanjo hiyo kusitishwa.