array(0) { } Radio Maisha | Wabunge na maseneta watoa risala za rambiramba kwa Mzee Moi

Wabunge na maseneta watoa risala za rambiramba kwa Mzee Moi

Wabunge na maseneta watoa risala za rambiramba kwa Mzee Moi

Mabunge ya Kitaifa na Seneti yamefanya vikao maalumu vya kutuma risala za rambirambi kufuatia kifo cha Mzee Daniel Toroitich Arap Moi huku yakilazimika kuaihirisha vikao vyao hadi Juma lijalo kuwapa nafasi Wabunge na Maseneta kuomboleza kifo cha rais huyo wa pili.

Maspika Ken Luska na Justine Muturi wameongoza vikao hivyo huku Muturi akiwapa dakika moja kila mbunge kutuma risala zake kwa familia ya Moi. Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa,  Aden Duale ambaye alikuwa wa kwanza kuzungumza, amememtaja Moi kuwa kiongozi aliyejitolea kuboresha maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa, Benjamin Cheboi amesema Moi alikuwa mstari wa mbele kuimarisha elimu na kuelezea jinsi alivyompa fursa ya kipekee ya kuabiri ndege yake.

Naye Mbunge wa Kiminini Dakta. Chris Wamalwa, amesema daima Moi atakumbukwa kwa kukubali kuachia madaraka mwaka wa 2002 huku akiwataka viongozi wengine kuiga mfano huo.

Mabunge yote yameafikiana kueahirishwa vikao hadi Juma lijalo Februari 13.

Wabunge wengine wa kike kwa kiume wamemmiminia sifa Hayati Mzee Moi.

Katika Bunge la Seneti, Spika Ken Lusaka alikuwa wa kwanza kutoa heshima zake kwa Mzee Moi.

Kiongozi wa Wawache katika Bunge la Seneti James Orengo amesema kuwa ni wajibu wa viongozi kuiga mfano wa Moi ambaye alihakikisha kuwa Wakenya wote wanaungana pasi na kujali matabaka wala  kabila. Orengo amesisitiza umuhimu wa maridhiano akisema ndio njia pekee ya kukuza taifa lenye amani.

Maseneta wakiwamo Moses Wetangula, Mutula Kilonzo Jnr,Yusuf Haji, Amos Wako, Mohammed Mohamud, Margret Kamar miongoni mwa wengine wamemtaja Moi kuwa mwanzilishi wa vyama vingi vya kiasiasa, mpenda watoto na hasa elimu ya mtoto wa kike.