array(0) { } Radio Maisha | Bunge kurejelea vikao vyake wiki ijayo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Bunge kurejelea vikao vyake wiki ijayo

Bunge kurejelea vikao vyake wiki ijayo

Matayarisho ya bajeti ya kitaifa ya mwaka 2020/21 pamoja na Mpango wa Upatanishi, BBI ni miongoni mwa masuala makuu yanayotarajiwa kutawala vikao vya wabunge watakaporejelea vikao vyao wiki hii.

Wabunge na Maseneta walitarajiwa kurejelea vikao vyao kesho kabla ya tarehe hiyo kusitishwa hadi Alhamisi ili kutoa fursa kwa viongozi hao kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais Hayati, Daniel arap Moi ambaye alifariki dunia katika Hospitali ya Nairobi Jumanne wiki iliyopita.

Hata hivyo, mabunge yote mawili yanatarajiwa kukutana leo kuidhinisha kuhairishwa kwa vikao hivyo, kwa mujibu wa sheria.

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Aden Duale amesema kikao cha leo vilevile kitatumia kuwasilisha majina ya Mawaziri Mutahi Kagwe wa Afya na Betty Maina wa Biashara na Viwanda ambao wanatarajiwa kupigwa msasa baada ya kuteuliwa kuhudumu na Rais Uhuru Kenyatta.

Aidha, inatarajiwa kwamba wabunge na maseneta watatumia vikao vya leo kutuma risala zao kwa familia ya Moi ambaye amewacha historia ya kuwa Mbunge aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika wadhifa huo ikiwa ni miaka 47 ikizingatiwa kwamba alichanguliwa mwaka wa 1955 katika bunge lililokuwa chini ya utawala wa wakoloni hadi mwaka 2002 alipojiuzulu.