array(0) { } Radio Maisha | Wakenya wautazama mwili wa Hayati, Daniel arap Moi

Wakenya wautazama mwili wa Hayati, Daniel arap Moi

Wakenya wautazama mwili wa Hayati, Daniel arap Moi

Rais Uhuru Kenyatta amewaongoza Wakenya kuutazama mwili wa aliyekuwa Rais wa Pili wa Kenya Hayati Daniel Arap Moi. Rais Kenyatta alifika katika majengo ya Bunge dakika chache baada ya saa nne asubuhi ambapo aliutazama mwili wa Hayati Moi akiwa amendamana na Mkuu wa Majeshi Jenerali samson Mwathethe na Mkewe Margaret Kenyatta.

Kisha akafuata Naibu wa Rais William Ruto ambaye aliwapisha mawaziri na wageni mbalimbali wakiwamo mabalozi, kabla ya kuwapisha viongozi wengine wakiwamo, magavana, maseneta na wabunge. Kwa sasa Wakenya wa Matabaka mbalimbali wanaendelea kuutazama mwili huyo shughuli itakayoendelea kwa siku tatu hadi Jumatatu.

Wakati uo huo, Rais amelihutubia taifa kwa mara ya kwanza tangu kutangaza kifo cha Hayati Moi. Rais Kenyatta amesema Hayati Moi, alikuwa rais ambaye alijitolea kuhakikisha kwamba taifa hili linasalia imara.

Rais ambaye alikuwa ameandamana na Naibu wake William Ruto katika Ikulu ya Nairobi, amesema Hayati Moi, alikuwa mwenye Demokrasia hasa baada ya kuukumbatia utawala wa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa.

Amesema hatua yake ya kuondoa ofisini bila mvutano wowote baada ya uchaguzi mkuu wa mwka 2002 ni wa kuigwa na viongozi wengien walio mamlakan.

Amesema atakumbukwa si tu humu nchini bali katika mataifa mengi ya bara Afrika kutokana na juhudi zake za kuhakikisha kunakuwapo na ushirikiano.

Hayati Moi aliyefariki dunia Jumanne wiki hii atazwa Jumatano wiki ijayo nyumbani kwake Kabarak kwenye Kaunti ya Nakuru. Ikumbukwe ibada ya wafu kwa ajili yake itafanyika Jumanne  ijayo katika uwanja wa Moi Kasarani jijini Niarobi. Ikumbukwe seriklai ilitangaza siku hiyo kuwa ya Mapumziko ya Kitaifa ili kuwapa nafasi Wakenya kumwomboleza kiongozi huyo shupavu.