array(0) { } Radio Maisha | Watu 4 wafariki dunia baada ya kufukiwa chimboni, Kaunti ya Migori

Watu 4 wafariki dunia baada ya kufukiwa chimboni, Kaunti ya Migori

Watu 4 wafariki dunia baada ya kufukiwa chimboni, Kaunti ya Migori

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Wachimbaji migodi wanne wamefariki dunia baada ya kufukiwa chimboni eneo la Osiri, kwenye Kaunti ya Migori.

Wenzao kumi na sita wanaendelea kuuguza majeraha mabaya sita miongoni mwao wakiwa katika hali mahututi.

Chifu wa eneo hilo David Oulo amesema kwamba mkasa huo ulitoka jana jioni kwenye mgodi huo kwa jina Osiri mines katika Kaunti ndogo ya Nyatike.

Kufikia mapema Alhamisi, kulikuwa na hofu kwamba hunda wachimbaji migodi zaidi walikuwa wamefukiwa chimboni humo.

Aidha, Chifu huyo amesema kwamba idadi ya waliokuwa ndani ya chimbo hilo haijulikani na kwamba waliofariki dunia walikosa hewa ya kupumua baada ya kuta za migodi hiyo kuporomoka na kuwazika wakiwa hai.