array(0) { } Radio Maisha | Uhuru kukutana na Trump tena

Uhuru kukutana na Trump tena

Uhuru kukutana na Trump tena

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Rais Uhuru Kenyatta Alhamisi anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya Marekani - White House. 

Hii itakuwa mara ya pili kwa viongozi hao kukutana baada ya ziara ya mwaka 2018  ambapo wawili walianza mazungumzo  ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

Trump anatarajiwa kutangaza mkataba mpya na Kenya kuhusu utakaotoa nafasi zaidi kwa bidhaa za Kenya kuuzwa Marekani kwa urahisi.

Kwa mujibu wa Trump, ushirikiano kati ya Marekani na Kenya utakuwa mfano wa ushirikiano sawa na huo na matifa mengine baadaye huku taifa hilo likilenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na mataifa ya Afrika.