array(0) { } Radio Maisha | Maandalizi ya hafla ya mazishi ya Moi yashika kasi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Maandalizi ya hafla ya mazishi ya Moi yashika kasi

Maandalizi ya hafla ya mazishi ya Moi yashika kasi

Na Mike Nyagwoka,

NAIROBI, KENYA, Ikiwa ni siku ya tatu ya maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Pili wa Taifa hili Hayati Daniel arap Moi, serikali Alhamisi inatarajiwa kutangaza kuhusu maandalizi ya hafla ya mazishi. Kamati andalizi ya hafla hiyo chini ya uongozi wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua atakayeongoza kikao hicho.

Ikumbukwe kamati hiyo ilikutana kwa mara ya kwanza Jumatano huku mipango ya hafla hiyo ya kitaifa ikiwa imeshika kasi.

Mazishi ya Hayati Moi yatakuwa ya pili kuandaliwa kwa namna ya kipekee huku wanajeshi wakitarajiwa kuongoza mara ya mwisho kwa hafla kama hii kufanyika ilikuwa wakati wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa taifa hili Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Ikizingatiwa kwamba Moi hakufariki dunia akiwa ofisini kutakuwapo na makombora ishirini na moja yatakayofyatuliwa angani wakati wa hafla hiyo. Hata hivyo, inawezekana mwelekeo utolewe kwamba azikwe kwa hadhi ya Mkuu wa Majeshi kufuatia uongozi wake wa miaka ishirini na minne basi atavalishwa sare kisha risasi ishirini na moja kufyatuliwa angani.

Inaarifiwa mwili wa Moi utapelekwa katika majengo ya bunge Jumanne kisha katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi ili kutoa fursa kwa umma kuutazama kabla ya kuzikwa nyumbani wake Kabarak kwenye Kaunti ya Nakuru Jumatano juma lijalo.