array(0) { } Radio Maisha | EACC na DCI zachunguza uteuzi wa maafisa wa Serikali ya Kaunti ya Nairobi

EACC na DCI zachunguza uteuzi wa maafisa wa Serikali ya Kaunti ya Nairobi

EACC na DCI zachunguza uteuzi wa maafisa wa Serikali ya Kaunti ya Nairobi

Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC na Idara ya Upelelezi DCI,  imeanzisha upya uchunguzi kufuatia uteuzi katika serikali ya Kaunti ya Nairobi na mienendo ya baadhi ya maafisa.

Mkurugenzi Mkuu wa DCI George Kinoti amesema idara hiyo inachunguza madai ya ufisadi dhidi ya maafisa wa kaunti huku EACC ikiwaagiza kumi na wanne kufika mbele yake kuhojiwa.

Miongoni mwa walioagizwa kufika kwa EACC ni pamoja na walioteuliwa hivi majuzi na wengine waliofutwa kazi kisha kurejeshwa kazini na Gavana Mike Sonko. Aidha EACC inachunguza utaratibu uliotumika kumchagua Ann Mwenda kuwa Naibu Gavana.

Katika aliyomwandikia Katibu wa Kaunti Kinoti anataka kukabidhiwa ripoti ya mkutanano ulioafikia wakati wa uteuzi wa msimamizi wa wadi ya shughuli za kikazi kwenye eneo la Embakasi Mashariki, uteuzi wa Bodi ya Kukabili Biashara ya Pombe na wawakilishi wadi waliohudhuria mikutano kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Maafisa wengine wanaotarajiwa kuhojiwa ni Katibu wa Kaunti  Leboo Ole Morintat Waziri wa Barabara Mohamed Dagane Charles Kerich wa Ardhi na Mpango wa Jiji, Veska Kangongo wa Ugatuzi, Lucia Mulwa  wa Elimu na  Hitan Majevda wa Afya.

Wengine ni Newton Munene wa Teknolojia, Allan Igambi wa Fedha, Larry Wambua wa Mazingira, George Oswewea aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Mwezake wa Kilimo, Karen Nyamu miongoni mwa wengine.

Kwa muda mrefu mvutano umekuwapo baina ya Sonko na EACC huku gavana huyo akiishtumu kwa kuwa na njama ya kutaka kumharibia jina kutokana na madai mengi wanayochunguza dhidi yake.

Ikumbukwe Gavana huyo anakabiliwa na tuhuma za wizi wa shilingi milioni mia tatu hamsini na saba za umma.